Friday, January 27, 2012
BALAA! SERIKALI YASHUPAA MADAI YA MADAKTARI
Na. Aron Msigwa –MAELEZO
Serikali imewataka madaktari wote nchini walio kwenye mgomo kurejea katika vituo vyao vya kazi na kufanya kazi za utabibu ili kuokoa maisha ya wagonjwa.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hadji Mponda amesema serikali inatambua mchango walio nao wataalam wa afya katika utoaji wa huduma za afya nchini na inaendelea kuboresha maslahi yao.
Amesema serikali kwa kutambua mchango huo imekuwa ikiboresha maslahi yao na kuongeza nafasi za ajira kila mwaka kwa wataalam wenye sifa kutoka nafasi 1,677 za mwaka 2005/2006 hadi kufikia 9,391 katika mwaka huu wa fedha 2011/2012.
“Serikali inatambua mchango wa watumishi wa kada za afya nchini na ndio maana nafasi za ajira zimekuwa zikiongezeka kila mwaka hasa katika mwaka huu wa fedha 2011/2012”
Amefafanu kuwa madaktari kupitia Chama chao (MAT) wamewasilisha madai mbalimbali serikalini yakiwemo nyongeza ya posho ya kuitwa kazini baada ya kazi na madaktari kupewa nyumba za kuishi karibu na hospitali amesema kuwa serikali imekuwa ikifanya jitihada za kuboresha maslahi hayo ili kuwawezesha wataalam hao kutekeleza majukumu yao ikiwemo ujenzi wa nyumba 8 za madaktari kwa wilaya 18 pamoja na kufanya maboresho ya posho.
“Serikali imepata fedha kutoka Mfuko wa Dunia(Global Fund) kwa ajili ya kujenga nyumba za madaktari na kwa kuanzia wilaya 18 zilizo pembezoni zimechaguliwa kujengewa nyumba 8 kila wilaya kama hatua ya kuboresha upatikanaji wa nyumba”
Kuhusu malipo ya udhamini kwa madaktari wanaochukua mafunzo ya uzamili,Kuhamisha madaktari bingwa wenye mikataba ya Ajira na Hospitali ya Taifa Muhimbili, Posho ya mazingira hatarishi na ajira za madaktari amesema kuwa baada ya serikali kupandisha hadhi ya hospitali za mikoa kuwa hospitali za Rufaa za mikoa kumekuwa na umuhimu wa madaktari hao kwenda kufanya kazi katika hospitali hizo na kuongeza kuwa idadi ya udhamini wa madaktari katika mafunzo ya uzamili imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka.
Aidha kuhusu madai ya kutaka nyongeza za mishahara ya shilingi milioni 3.5 kwa mwezi Dkt. Mponda ameeleza kuwa mishahara ya watumishi serikalini hufuata miundo ya utumishi (Scheme of Service)iliyopo huku akibainisha kuwa muundo wa malipo ya watumishi wa umma katika sekta ya afya umeboreshwa.
“Lazima tukubali kuwa baada ya kuboreshwa kwa miundo ya utumishi wa umma wafanyakazi wa sekta ya afya hivi sasa wanapata mishahara mikubwa kuliko watumishi wengine serikalini” amesisitiza.
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ATEMBELEA MASHAMBA YA MPUNGA KOROGWE, AWEKA JIWE LA MSINGI JENGO LA UKUMBI NA OFISI YA HALMASHAURI YA KOROGWE
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka Jiwe la Msingi katika jengo jipya la Ukumbi na Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe, wakati alipokuwa katika ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo ya Wilaya ya Korogwe mkoa wa Tanga jana Januari 26, 2012.
Majambazi yapanga mawe na kupora manyoni
Ndugu zangu,
Niliondoka Singida Mjini saa kumi na moja alfajiri kuelekea Dodoma. Kilomita 40 kutoka Manyoni nilikutana na hali hiyo pichani kunako saa kumi na mbili na nusu. Eneo la tukio niliwakuta askari watano wamevalia kiraia wakiwa na silaha za moto. Wameniambia tukio limetokea usiku wa kuamkia leo majira ya kuanzia saa sita usiku na linawahusisha maja majambazi wasiopungua wanane.
Kuna walioporwa fedha, simu na mali zao . Mahali hapa kuna pori kubwa upande wa kushoto. Inaaminika majambazi hayo yenye silaha yangali yamejiicha porini.
Hakuna aliyekamatwa. Nilishuhudia polisi hao wakifuatilia nyayo huku wakinionyesha mahali majambazi hayo yalilala chini kujificha wakisubiri giza na kuanza kupanga mawe yao. Kwa kusoma mazingira ya eneo kwangu mimi napata tafsiri kuwa majambazi hayo yalifanya maandzi ya mpango wao kwa siku kadhaa.
Maana, mawe hayo mazito yanaonekana kuwa yalikuwa yakisogezwa usiku karibu na tukio na kufikia idadi waliyohitaji. Intelijensia ya kipolisi ingefanya kazi yake sawa sawa na kwa kushirikiana na wenyeji ingewezeza kubaini mapema movement ya mawe yale. Na katika dunia ya sasa , mbwa wa polisi waliopewa mafunzo wangefanya kwa haraka na kwa ufanisi zoezi la kufuatilia majambazi porini badala ya polisi kufuatilia nyayo kwa macho
mtoto waua Mbeya
MWANAMKE ASHITAKIWA KWA KOSA LA KUSABABISHA KIFO CHA MWANAE
Habari na Mwandishi wetu
Neema Edson mwenye umri wa miaka 19 mkazi wa Namtanga Swaya jijini Mbeya amefikishwa katika mahakama ya mkoa kwa kosa la kumuua mtoto wake akiwa mchanga.
Akisoma shitaka hilo mbele ya hakimu mkazi mfawizi Monika Ndyekobola mwanasheria wa serikari Ema Msofe amesema mshtakiwa alitenda kosa hilo January 3 mwaka huu maeneo ya namtanga jijini hapa.
Amemtaja mtoto aliyeuawa kuwa Steven Chinga ambaye alikuwa na umri chini ya miezi kumi na miwili kinyume na kifungu cha sheria namba 199 sura ya 16 kama kilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Hata hivyo mshtakiwa hakutakiwa kujibu lolote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na dhamana ya kusikiliza kesi kama hizo na kesi hiyo itaanza kusomwa upya februari 6 mwaka huu katika mahakama kuu.
Neema Edson mwenye umri wa miaka 19 mkazi wa Namtanga Swaya jijini Mbeya amefikishwa katika mahakama ya mkoa kwa kosa la kumuua mtoto wake akiwa mchanga.
Akisoma shitaka hilo mbele ya hakimu mkazi mfawizi Monika Ndyekobola mwanasheria wa serikari Ema Msofe amesema mshtakiwa alitenda kosa hilo January 3 mwaka huu maeneo ya namtanga jijini hapa.
Amemtaja mtoto aliyeuawa kuwa Steven Chinga ambaye alikuwa na umri chini ya miezi kumi na miwili kinyume na kifungu cha sheria namba 199 sura ya 16 kama kilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Hata hivyo mshtakiwa hakutakiwa kujibu lolote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na dhamana ya kusikiliza kesi kama hizo na kesi hiyo itaanza kusomwa upya februari 6 mwaka huu katika mahakama kuu.
Tuesday, January 3, 2012
Subscribe to:
Posts (Atom)