Karibuni NL Internet C@fe kwa huduma safi ya internet yenye kasi ya 5mbps kupandisha na kushusha.Tupo Tabata CCM,mkabala na kituo cha mafuta cha OILCOM.

Friday, September 16, 2011

Chadema wamkamata Mkuu wa Wilaya Igunga


Msafara wa Chadema ulifika katika eneo la kampeni saa 8.00 mchana na kabla mkutano haujaanza, Meneja Kampeni wa chama hicho, Sylivester Kasulumbai, aliwaambia waandishi wa habari kuwa mkuu wa wilaya ya igunga alikuwa akifanya kikao cha ndani katika eneo hilo kinyume na taratibu, hivyo wanakwenda kumshughulikia.

Kasulumbai ambaye ni Mbunge wa Maswa Mashariki akiwa na Mbunge wa Viti Maalum, Susan Kiwanga, baadhi ya wananchi na vijana wao, walifika katika ofisi ya Mtendaji wa Kata kulikokuwa kunafanyika mkutano huo na kuanza kuhoji aliko Mkuu huyo wa Wilaya.

Mmoja wa wananchi alimnyooshea kidole mama ambaye alikuwa amekaa mbele na kusema; “..yule ndiye Mkuu wa Wilaya”.Kundi hilo la vijana na viongozi wa Chadema, waliingia katika ukumbi huo na kumtoa nje mama huyo huku wakimtaka aeleze kwa nini anafanya vikao vya ndani katika Kata hiyo wakati anajua kuwa chama hicho kilikuwa na mkutano katika eneo hilo.

Kitendo hicho kilizua purukushani na kutokuelewana kati ya waliokuwa kwenye mkutano wa ndani na viongozi wa Chadema, jambo lililovuta umati mkubwa wa watu.

Maelezo ya DC
Baadhi ya vijana wa Chadema walikuwa wamewashikilia watu waliokuwa wakishiriki mkutano huo huku mama huyo ,gonga hapa kusoma zaidi

Mambo ya Kampeini haya


Kampeini za igunga ..... ni matambo matupu...

SOKO LA SIDO LAUNGUA MOTO



huu ni moshi wa soko la SIDO kuliko kuwa kambi ya SUGU kipindi cha kampeini za uchaguzi mkuu.