Karibuni NL Internet C@fe kwa huduma safi ya internet yenye kasi ya 5mbps kupandisha na kushusha.Tupo Tabata CCM,mkabala na kituo cha mafuta cha OILCOM.

Saturday, May 19, 2012

PREDECT PLZ

MAY GOD BE WITH CHELSAEFC

Mtoto wa Ajabu -songea

MTOTO mwenye maumbile ya ajabu akiwa na jinsia mbili za kiume na moja ya kike amezaliwa Aprili 25 mwaka huu majira ya saa 11 jioni katika hospitali ya mkoa wa Ruvuma mjini Songea. Mtoto huyo ambaye bado yupo hai chini ya uangalizi maalum amezaliwa akiwa na hitilafu katika maumbile yake ikiwa ni pamoja na kuzaliwa na nusu ya ubongo ambayo imetokana na hitilafu kwenye mfumo wa kichwa hadi uti wa mgongo. Muuguzi wa zamu katika wodi ya wazazi katika hospitali ya mkoa ambako mtoto huyo anaangaliwa Agness Mwinuka amesema mtoto huyo ambaye amezaliwa na uzito wa kilo moja na gramu 900 amezaliwa akiwa na jinsia mbili za kiume na jinsia moja ya kike. “Jinsia moja ya kiume ipo kama kawaida isipokuwa jinsia moja ya kiume ipo kichwani karibu na kisogo na jinsia ya kike ipo utosini, mtoto huyu tangu azaliwe juzi hadi sasa hana uwezo wa kunyonya wala kula kitu chochote, uchunguzi wa kitabibu bado unaendelea’’,alisisitiza. Mama mzazi wa mtoto huyo Situmahi Mwinuka(32) mkazi wa Msamala mjini Songea anasema huyu ni mtoto wake wa nne kuzaliwa na kwamba watoto wake wengine watatu hawajawahi kupata hitilafu yeyote katika mwili. Kaimu mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Ruvuma Dk.Mathayo Chanangula akielezea hali ya mtoto huyo alisema mtoto anakabiliwa na tatizo ambalo kitaalam ni hitilafu kwenye mfumo unaoanzia kichwani hadi kwenye uti wa mgongo ambao umesababisha mtoto huyo kuzaliwa na nusu ya ubongo. Kulingana na daktari huyo hitilafu hiyo imesababisha mifumo ya mwili kuwa na dosari ambapo kuna sehemu mbili za kiume moja ikiwa kichwani na kwamba mtoto anapolia sehemu ya kiume ya kichwani inasimama na kusisitiza kuwa maisha ya mtoto huyo ni mafupi kutokana na mifumo ya mwili wake kutokamilika licha ya kwamba mtoto amezaliwa na miezi tisa. “Katika nchi zilizoendelea madaktari bingwa na wenye vifaa vya kisasa wanaweza kuokoa maisha ya mtoto huyo,hata kama mtoto huyo anaokolewa atakabiliwa na tatizo kubwa la ulemavu wa akiri kwa kuwa ubongo alionao ni nusu tu ya ubongo unaotakiwa kwa binadamu kamili’’,alisisitiza. Dk. Chanangula anabainisha kuwa mama mjamzito anaweza kujifungua mtoto mwenye maumbile ya ajabu iwapo atakosa madini aina ya folic acid ambayo alisisitiza ni muhimu kwa mama mjamzito kunywa madini hayo miezi mitatu ya mwanzo ya ujauzito wake. “Mama anaweza kujifungua mtoto mwenye maumbile ya ajabu iwapo katika miezi mitatu ya mwanzo katika ujauzito wake atatumia dawa aina ya flagile, dawa za minyoo, tetesakline na baadhi ya dawa za malaria kama vile SP ambayo anaruhisiwa kunywa baada ya wiki 28 na ALU ambayo hairuhusiwi kabisa kutumika kwa mjamzito kwa ujumla ni marufuku mama mjamzito kunywa dawa bila kumuona daktari’’,alisisitiza. Katika hospitali ya mkoa wa Ruvuma hili ni tukio la kwanza la aina yake mtoto kuzaliwa akiwa na hitilafu kubwa katika mifumo ya mwili wake. Habari hii imeandikwa na Albano Midelo

Sunday, May 6, 2012

BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI HILI HAPA WAZEE

===== ===== === TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI ORODHA YA MAWAZIRI NA NAIBU MAWAZIRI MAWAZIRI 1. OFISI YA RAIS Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu) Ndugu Stephen M. Wasira, Mb., Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, (Utawala Bora) Ndugu George Mkuchika, Mb., Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (UTUMISHI) Ndugu Celina Kombani, Mb., 2. OFISI YA MAKAMU WA RAIS Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (MUUNGANO) Ndugu Samia H. Suluhu, Mb., Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (MAZINGIRA) Dr. Terezya P.L. Huvisa, Mb., 3. OFISI YA WAZIRI MKUU Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji) Ndugu Mary M. Nagu, Mb., Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) Ndugu Hawa Ghasia, Mb., Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Ndugu William V. Lukuvi, Mb., 4. WIZARA Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Ndugu Samuel J. Sitta, Mb., Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Ndugu Shamsi Vuai Nahodha, Mb., Waziri wa Ujenzi Dr. John P. Magufuli, Mb., Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Hussein A.H. Mwinyi, Mb., Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dr. Shukuru J. Kawambwa, Mb., Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Ndugu Sophia M. Simba, Mb., Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Ndugu Bernard K. Membe, Mb., Waziri wa Katiba na Sheria Ndugu Mathias M. Chikawe, Mb., Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Ndugu Emmanuel Nchimbi, Mb., Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dr. David M. David, Mb., Waziri wa Kazi na Ajira Ndugu Gaudentia M. Kabaka, Mb., Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame M. Mbarawa, Mb., Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna K. Tibaijuka, Mb., Waziri wa Maji Prof. Jumanne Maghembe, Mb., Waziri asiyekuwa na Wizara Maalum Prof. Mark Mwandosya, Mb., Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Eng. Christopher Chiza, Mb., Waziri wa Uchukuzi Dr. Harrison Mwakyembe, Mb., Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dr. Fenella E. Mukangara, Mb., Waziri wa Maliasili na Utalii Ndugu Khamis Kagasheki, Mb., Waziri wa Viwanda na Biashara Dr. Abdallah O. Kigoda, Mb., Waziri wa Fedha Dr. William Mgimwa, Mb., Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo, Mb., 5. NAIBU MAWAZIRI OFISI YA RAIS HAKUNA NAIBU WAZIRI 6. OFISI YA MAKAMU WA RAIS Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais Ndugu Charles Kitwanga, Mb., 7. OFISI YA WAZIRI MKUU Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) Ndugu Majaliwa K. Majaliwa, Mb., Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) Ndugu Aggrey Mwanry, Mb., 8. WIZARA MBALIMBALI Naibu Waziri wa Kazi na Ajira Dr. Makongoro M. Mahanga, Mb., Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Ndugu Adam Malima, Mb., Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Ndugu Pereira A. Silima, Mb., Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Ndugu Gregory G. Teu, Mb., Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Ndugu Benedict N. Ole-Nangoro, Mb., Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Ndugu Mahadhi J. Maalim, Mb., Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Ndugu Goodluck J. Ole-Medeye, Mb., Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Ndugu Ummy A. Mwalimu, Mb., Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Ndugu Philipo A. Mulugo, Mb., Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dr. Abdulla Juma Abdulla, Mb., Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Ndugu Lazaro Nyalandu, Mb., Naibu Waziri wa Ujenzi Ndugu Gerson Lwenge, Mb., Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dr. Seif Suleiman Rashid, Mb., Naibu Waziri wa Nishati na Madini Ndugu George Simbachawene, Mb., Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Ndugu January Makamba, Mb., Naibu Waziri wa Uchukuzi Dr. Charles J. Tizeba, Mb., Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Ndugu Amos Makala, Mb., Naibu Waziri wa Maji Eng. Dr. Binilith Mahenge, Mb., Naibu Waziri Nishati na Madini Ndugu Stephen Maselle, Mb., Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Ndugu Angela Jasmine Kairuki, Mb., Naibu Waziri wa Fedha Ndugu Janet Mbene, Mb., Naibu Waziri wa Fedha Ndugu Saada Mkuya Salum, Mb., Imetolewa na: Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu. Dar es Salaam. 4 Mei, 2012