Karibuni NL Internet C@fe kwa huduma safi ya internet yenye kasi ya 5mbps kupandisha na kushusha.Tupo Tabata CCM,mkabala na kituo cha mafuta cha OILCOM.

Friday, September 10, 2010

Ujumbe wetu wa leo

YANAYOWEZA KUKUSAIDIA KUTIMIA NDOTO ZAKO – 2

 

Naanza kwa kumshuku Mungu kwa upendo aliouonyesha kwangu na kuniwezesha kuiona siku hii ya ya leo nikiwa mzima wa afya. Nadiriki kushukuru kwa sababu, wapo walitamani kuiona wiki hii wakiwa wazima lakini wengine waneshatangulia mbele za haki huku wengine wakiwa hoi mahospitalini na majumbani.

 

Mimi na wewe ambao tumejaaliwa uhai hadi leo, tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu na pia kujaribu kubadilika na kujitahidi kufanya yale ambayo yatamfurahisha na kuachana na yale yatamchukiza.

 

Wiki iliyopita nilianza kuzungumzia mambo ambayo yanaweza kumsaidia mtu kutimiza ndoto zake, wiki hii nitamalizia mambo kadha yaliyobaki.

 

JIPANGE

Baada ya kuorodhesha malengo yako katika maisha. Unashauriwa kutafakari na kutafuta hayo. Hapa nazungumzia suala zima la maandalizi ambayo ytakusaidia kufikia ndoto zako kwa usahihi na kwa haraka.

Kama malengo yako yatahitaji mtaji wa kutosha basi itakulazimu kutafuta pesa kwa nguzu zote na kama itakuhitaji kuwa na elimu ya kutosha huna budi kujibadilisha katika hilo.

 

USIOGOPE KUJARIBU

Maisha siku zote wana msemo ni mapambano na kujitoa mhanga. Maisha ni kujitolea na kutoogopa kujaribu kwa kuhofia kushindwa. Kamwe usiogope kujaribu kwani hata ikitokea ukashindwa bado kwako itakuwa ni changamoto na njia ya kujifunza maisha zaidi.

TUMIA MUDA WAKO VIZURI

Wenzetu wazungu msemo wao usemao “Time is money” ni kweli, muda ni hazina na asilimalinyeti sana katika kufanikisha malengo yako ya kimaisha. Jitahidi sana kutumia muda wako vizuri badala ya kuupoteza katika mambo ambayo hayatakusaidia katika maisha.

JIFUNZE KWA WENGINE

Kuwa tayari kutoka kwa wengine ambao wamefanikiwa katika kile unachotamani kukifanya. Jaribu kudadisi na kung’amua ni kwa namna gani wameweza kufikia malengo yao  katika maisha ili na wewe uweze kujifunza kitu.

USIKATE TAMAA

Katika kujaribu kufikia malengo yako ni wazi kuwa utakutana na vikwazo vya hapa na pale na wakati mwingine kuweza kuhisi huwezi kuendelea tena.

 

Siku zote vikwazo unavyokutana navyo view ni changamoto kwako ya kujipanga upya na kuanzisha tena mapambano ya kufikia malengo yako. Kimsingi hushauriwi kukata tama kabisa kwani wataalamu wa mambao ya saikolojia wanaeleza kuwa, idadi kubwa ya watu wanaoishi maisha yasiyokuwa na nyuma wala mbele wametawaliwa na tabia ya kukata tama hata katika mambo ambayo wakiwa wavumilivu wanaweza kufanikiwa.

OMBA MSAADA, USHAURI IKIBIDI

Kujiamini ni mambo ya msini sana kwa kila mwenye uchu na maendeleo lakini ukweli unabaki pale pale kwamba, huwezi kufanya kila kitu wewe mwenyewe. Katika mbio za kufikia malengo yako, usiishi kama  kisiwa, wakati mwingine itakuhitaji kuomba msaada au hata ushauri wa kimawazo pale utakapotingwa na mambo. Usikubali kubaki na msongo wa mawazo pale unapohisi kushindwa badala yake jaribu kutafuta msaada na ushauri kwa watu unawaamini.

JIHADHARI NA ANASA

Ulevi na kuendekeza kabla ya kufikia malengo yako kimaisha ni kikwazo kikubwa cha kujitakia na ni sumu mbaya ya fedha na kupoteza muda mwingi katika mambo ya anasa kamwe hayataweza kukusaidia kutimiza ndoto zako. Daima kazi kwanza,starehe baadae, ishi kama mtumwa leo, ili utimie ndoto ya kuishi kama mfale kesho

JITATHMINI

Katika hatua nyingine ni vyema pia ukachukua muda wako kutathmini namna ambavyo umeweza kutekeleza malengo yako, hii ni pamoja na kuweza kufahamu maendeleo yako katika mpango wa kufikia malengo yako, ni kwa kiasi gani umeweza kufanikiwa pia ni kiasi gani umeshindwa na kwa nini.

Kwa kufanya hivi inaweza kukusaidia kuweza kutilia mkazo zaidi katika maeneo yalioonesha udhaifu na kurekebisha kasoro kadhaa lakini pia kujipanga kwa nguvu mpya ili kutimiza ndoto zako kwa ufanisi zaidi.

 

Nimefikia tamati, tuonane tena wiki ijayo kwa mada nyingine.

No comments:

Post a Comment