Karibuni NL Internet C@fe kwa huduma safi ya internet yenye kasi ya 5mbps kupandisha na kushusha.Tupo Tabata CCM,mkabala na kituo cha mafuta cha OILCOM.

Monday, November 7, 2011

PSPF YAKABIDHI MSAADA KWA KIKUNDI CHA WALEMAVU CHANG'OMBE



Ofisa Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa Mashirika ya Umma (PSPF), Bi.Fatma Elhady (kushoto), akimkabidhi msaada wa hundi ya shilingi milioni 1.5 Bi.Dominion Apiyo wa Kikundi cha Walemavu cha Little cha Chang'ombe wilayani Temeke ,Dar es Salaam jana.

huu Unyama wa hawa wanao amini imani potofu utakwisha lini? kwetu kuna Serikali kweli?




Msichana Kulwa Lusana ( 16 ) mwenye ulemavu wa ngozi (Albino ) mkazi wa kijiji cha Mbizi, Kata mpya ya Mbega iliyozaliwa kutoka Kata ya Segese wilayani Kahama mkoani Shinyanga, akiwa amelazwa katika wodi ya majeruhi katika hospitali ya wilaya ya Kahama baada ya kufanyiwa ukatili na unyama kwa kukatwa mkono wake wa kulia saa saba usiku wa kuamikia Jumamosi, Oktoba 22 mwaka huu akiwa amelala nyumbani kwa wazazi wake na watu wasiojulikana ambao waliondoka na mkono wake.